Friday, November 14, 2008

Mambo vipi marafiki wapendwa! Mimi sijambo hofu kwenu tu! Karibuni tena katika majaribio yetu ya kurusha habari za uhakika toka sehemu mbalimbali duniani, kwa sasa unaweza kupata habari yeyote ile uitakayo kutoka nje ya Bongo kupitia blog hii. Angalia headlines za habari hizo upande wako wa kulia wa monitor yako!
Marafiki, bado tupo kwenye maandalizi ya kuwaletea habari na burudani motomoto! Tafadhali endelea kuwa nami................! kwa sasa pata habari mbalimbali za kimataifa ikiwemo uchumi, sayansi, siasa, michezo na burudani kupitia blog hii upande mdogo wa kulia wa monitor yako.





Ujumbe wetu wa leo unasema hivi.....................

usiamini kwa kuona wala kugusa, amini kwa vipimo!

Cial..................

emmanueljames18@yahoo.com/emmanueljms1@gmail.com



Jamani kwa wale wenye wenza (mke/mume), hali hii inatisha sana, na chanzo cha haya yote ni ama talaka au kutokuwa na maelewano baina yenu. Sasa kama huna mnyama anayeweza kutoa maziwa ya kutosha kwa mwanao unadhani nini kitatokea? Pia wale wenye wafanyakazi wa ndani ni-vema mkaishi nao vizuri ikiwa ni pamoja na kuwatimizia haki na mahitaji yao ya msingi ili kuepuka vitu kama hivi kwakuwa muda mwingi upo mbali na familia na hujui nini kinatokea wakati haupo.
Ingetokea hapa bongo pakawa na gari ndogo (tax) za aina hii, basi daladala zisingesumbua mijini kiasi hiki na huenda ajali zingepungua kwa kiasi fulani.


Hawa ni baadhi tu ya watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu, ambapo huishi chini ya dola moja kwa siku au hata kwa wiki! Kwa hali ya kawaida mtoto kama huyu akili yote inawaza pesa, sasa je iwapo atapata nafasi ya kuwa maeneo ya pesa atafanya nini?



Inaonekana biashara ya vyuma chakavu bado haijaingia eneo hili au haina soko. Unafikiria nini rafiki iwapo pikipiki kama hii itawekwa vibaya maeneo ya huku bongo?

Thursday, November 13, 2008

Bila shaka iwapo watoto wetu wangekuwa bize kiasi hiki, basi nadhani swala la ufisadi lisingekuwepo. Lakini swala la mtoto kuzaliwa kaliakoo na kukulia manzese ni moja kati ya sababu kubwa zinazoongeza ufisadi. Hii ni sawa na mtoto asiyepata chakula mara kwa mara sasa ikitokea kakiona chakula basi atachukua kwa mikono yote miwili ili wengine wasipate.